Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuzitunza vizuri Kadi zao za Kupiga Kura. Zipo taarifa zinazotolewa na baadhi ya Vyombo vya Habari kuwa kuna baadhi ya watu wanapita kuwataka watu waliojiandikisha kuwapa Kadi zao za kupiga Kura. Tume inawatahadharisha wananchi kuwa lengo la watu wanaochukua Kadi za Wapiga Kura sio zuri hivyo wasitoe kadi za mpiga kura kwa mtu yeyote. Ikumbukwe kwamba Kadi ya Mpiga imetolewa kwa madhumuni ya kupiga Kura siku ya tarehe 25 Oktoba, 2015. Ni kosa kwa mtu kumtaka mpiga kura kumpa kadi yake ya kupiga Kura. Ni kosa kwa mtu aliyejiandikisha kutoa au kugawa kadi yake ya kupiga Kura kwa mtu yeyote. Watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria. Kila mtu aitunze kadi yake mahali pazuri na kuitumia siku ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015. Mtu hataweza kupiga Kura kama atakuwa hana kadi ya kupiga Kura. Kadi ya kupiga Kura uliyopewa siku uliyojiandikisha ni Mali yako na sio Mali ya mtu mwingine. TUNZA KADI YAKO ILI UPIGE KURA

Comments

Popular Posts